Ligi Kuu Barainatarajiwa kuendelea kesho kwa
michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi
ya tisa huku kila timu ikisaka ushindi wa pointi tatu muhimu.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC
watawakaribisha Coastal Union kutoka jijini Tanga, mchezo utakaonza majira ya
saa 10:30 jioni, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand United uwanja wa
Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Wachimba Almasi wa Mwadui FC watawakaribisha Yanga SC
katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Toto African watakua wenyeji wa
maafande wa Mgambo Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar watakua wenyeji
wa Kagera Sugar katika uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, huku watoza
ushuru wa jiji la Mbeya katika uwanja wa Sokoine Mbeya City watakua wenyeji wa
Majimaji kutoka mkoani Ruvuma.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa michezo
miwili kuchezwa, Tanzania Prisons watakua wenyeji wa African Sports katika
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, JKT Ruvu watakua wenyeji wa Azam FC katika
uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment