October 27, 2015


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema wataifunga Coastal Union na kurejea katika hali yao.


Kerr amesema kikosi chao hakijayumba kiasi cha kuonekana kimeshindwa sana baada ya kupoteza mechi dhidi ya Prisons.

“Lakini watu wamefanya ionekane kama tupo katika hali ngumu sana. Tunaendelea kupambana na tutawafunga Coastal Union ili turudi katika hali yetu.

“Siwezi kusema hatuwaheshimu, lakini tunachotaka ni ushindi,” alisema Kerr.

Simba inakutana na Coastal Union kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Kikosi hicho cha Kerr kipo katika nafasi ya tano kikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi saba na kupotez ambili dhidi ya Yanga na Prisons ya Mbeya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic