October 27, 2015


Wakati Azam FC inashuka dimbani kuivaa African Sports keshokutwa Alhamisi, Kocha Stewart Hall amesema anataka mabao zaidi.

Katika mechi zake saba za Ligi Kuu Bara, Azam FC ambayo iko katika nafasi ya pili imefunga mabao 11.

Azam FC ina pointi 19 sawa na Yanga, lakini inazidiwa mabao saba ya kufunga, hali inayomfanya Kocha Stewart Hall atake mabao mengi zaidi ya kufunga.

“Mabao mengi ya kufunga ni jambo zuri zaidi, katika ligi kila kutu chenye faida unatakiwa kuwa nacho.
“Unaona Yanga wanafaidika na mabao ya kufunga kwa sasa. Nimezungumza na wachezaji na hilo pia tunalifanyia kazi.
 
HALL (KULIA) AKIWA NA KOCHA MKUU WA YANGA, ERNIE BRANDTS.
“Muhimu sana kuzitumia nafasi tunazotengeneza kwa ajili ya kufunga mabao mengi,” alisem Hall.

Hata hivyo, kikosi cha Hall raia wa Uingereza ni kati ya vile vyenye safu ngumu ya ulinzi kwa kuwa Azam FC na Yanga ndiyo timu zilizofungwa mabao machache zaidi. Kila moja imefungwa mabao matatu tu ndani ya mechi saba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic