October 2, 2015


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za pongezi kwa Alberto Simago Junior wa Shirikisho la Soka la Msumbiji (FMF) na Sidiki Tombi wa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT) kufuatia kuchaguliwa kuwa marais wa mashiriksho hayo.

Katika salam zake kwenda FMF na FECAFOOT, Malinzi amesema kuchaguliwa kwao kuogoza mashirikisho hayo kumetokana na imani ya wanafamilia wa mpira miguu.
Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya TFF na familia ya mpira wa miguu nchini, anawapa pongezi kwa kucgahuliwa kwao.
TFF inaahidi kushirikiana na uongozi mpya wa FMF na FECFOOT katika maendeleo ya mpira wa miguu Afrika na Dunia kote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic