Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo mchana
katika uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo dhdi ya Malawi utakaocheza Jumatano
Oktoba 7, 2015 kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini
Urusi.
Stars inayonolewa na kocha mkuu mzawa Charles Mkwasa, akisaidiwa
na Hemed Morroco, Peter Manyika na mshauri wa Ufundi Abdallah Kibadeni
wameingia kambini jana katika hoteli ya Urban Rose iliyopo Kisutu jijini Dar es Salaam.
Wachezaji
wote wameripoti kambini isipokuwa wachezaji wa kimataifa wanaocheza soka la
kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu
wanaotarajiwa kuungana na wenzao mwishoni mwa wiki baada ya kumaliza michezo
inayowakabili wikiendi hii.
Wachezaji
waliopo kambini ni magolikipa All Mustafa, Aishi Manula, Said Mohamed, walinzi
Juma Abdul, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Haji Mwinyi, Hassan Isihaka,
Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub “Cannavaro”.
Wengine
ni viungo Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Said Ndemla, Salum Telela,
Deus Kaseke, Saimon Msuva, Farid Musa, washambuliaji John Bocco, Rashid Mandawa
na Ibrahim Hajibu
0 COMMENTS:
Post a Comment