October 15, 2015


Mashabiki wa Hispania wamepiga kura na kumuweka mshambuliaji Diego Costa mguu ndani, mguu nje katika kikosi cha timu ya taifa.
Licha ya Costa kuwa mshambuliaji tegemeo, lakini inaonekana nafasi yake sasa ni ndogo baada ya kugawana kura na washambuliaji wengine.
Mshambuliaji kinda, Alavaro Morata ndiye ameonekana kuwa chaguo namba moja la mashabiki baada ya kumpa kura nyingi.

Costa ambaye msimu huu mambo yake si mazuri hata katika kikosi chake cha Chelsea, amegawana kura za ubora na washambuliaji Nolito na Pedro ambaye mashabiki wanataka acheze kama mshambuliaji wa pili nyuma ya Morata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic