Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Charles Boniface
Mkwasa ametangaza kikosi cha timu ya taifa kilicho tayari kupambana na Algeria.
Stars itaivaa Algeria katika mechi mbili mfululizo kuwania kucheza Kombe la Dunia 2018, ikianza kwa kupambana nayo Novemba 17 jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana Novemba 17, ugenini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena
jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini
Omani kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo huo.
Kikosi kamili alichokitaja Mkwasa kina wachezaji wapya sita ambao Salim Mbonde, Jonas Mkude,
Salum Abubakar, Malimi Busungu, Ramadhani Kessy na Elius Maguli na
kufanya idadi ya wachezaji 28.
Wachezaji
aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said
Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein
(Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam), Walinzi wa
kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na
nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo
ni Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank
Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa pembeni
Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars –
Afrika Kusini).
0 COMMENTS:
Post a Comment