October 18, 2015

....SIJUI ILIKUWAJE HAPA!

Soka ina burudani yake aisee, kama jana ulipata nafasi ya kwenda kwenye Tamasha la Kandanda Day utakubaliana nami.


Timu mbili za ushindani wa kindugu, timu Ismail na timu Dizzo zilichukuana vikali na kutoa burudani.
Mwisho washindi, Ismail wakashinda. Lakini mmoja wa memba wao, Nassor Bin Slum, yule mdhamini maarufu wa mambo ya michezo ambaye kampuni yake ya Bin Slum Tyres Ltd inayoongoza kwa kuuza matairi na betri za magari, naye alitia for a.

Maana alikuwa mbishi huyo, kila wakati analalamika, anamlalamikia mwamuzi, basi ili mradi kuwachanganya wenzake.

Kweli mbinu zake zilifanikiwa, timu yake yaani Team Ismail ikafanikiwa kuibuka na ushindi. Eeeeeh!

.....HAPA LAZIMA NI TIMBWILI NA MWAMUZI....

Hata hivyo, mwisho wa tamasha, alipewa tuzo kutokana na kuonyesha mchango wake na kudhamini tamasha hilo ambalo sasa linazoa umaarufu!



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic