December 6, 2020




INAELEZWA kuwa mshambuliaji namba moja ndani ya Simba, Meddie Kagere na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck haziivi chungu kimoja jambo linalomfanya ajenge ushkaji na benchi.


Hali hiyo inatajwa kuwa sababu ya Kagere kuweza kusepa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa hajui hatma yake itakuaje kwenye maisha yake ya kucheza ndani ya uwanja.


Kagere amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu ambapo inaelezwa kuwa alipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma ila aliitwa kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda.


Kwa msimu huu wa 2020/21 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikiwa imecheza mechi mbili na kutumia dakika 180 uwanjani, nyota huyo ametumia dakika mbili pekee.


Wakati ikishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau Uwanja wa New Jos, Kagere aliishia benchi huku mchezo wa pili Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikiambulia sare ya bila kufungana aliingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya John Bocco na kutumia dakika mbili ndani ya uwanja.


Suala hilo linatajwa kuwa sababu ya chanzo cha nyota huyo kufungua njia ya kusepa ndani ya kikosi hicho ambacho amekifungia jumla ya mabao 49 ndani ya ligi.


Vandenbroeck amesema kuwa wachezaji wake wote wana uwezo mkubwa wa kucheza na kila mmoja ana umuhimu wake.

18 COMMENTS:

  1. Kagere endelea kuvumilia tu mambo yatakaa sawa tu, wewe ndiye Okwi wetu kwa wanamsimbasi mabingwa wanchi na sasa mnapeperusha vyema benders ya nchi kimataifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kagere amekuwa akisumbuliwa na majeraha hivi karibuni hata alipoitwa kwenye timu yake ya taifa Amuvubi alishindwa kucheza acheni upumbavu.

      Delete
  2. Kama wote wana uwezo kwa nini hapewi nafasi sasa? Huyu kocha awe mkweli

    ReplyDelete
  3. Asepe tu huyu kishingo bado mwanafunzi wa ukocha analeta bifu zisizo na kichwa

    ReplyDelete
  4. Nyie mnaocomment humu hv mna akili timamu kweli? lini mmesikia Kagere ametamka kwa kinywa chake kwamba anataka kuondoka ndani ya simba. Pimeni kwanza habari zinazotolewa na hawa waandishi mtu anakurupuka tu anajitungia stori na nyinyi mnakuja na mihemko yenu, kaeni mkijua kuna waandishi wanatumika na timu pinzani kuchafua hali ya hewa ndani ya simba mara sijui Kagere kapigana na Sven yani stori za kutunga na washabiki wa simba nao wanaingia kwenye mkumbo huo huo acheni uzwazwa nyinyi washabiki wa simba, Kagere alikuwa majeruhi hana match fitness unataka acheze mechi na plateua watu wanatumia nguvu vile alafu baade mumlaumu kwa nini asingempanga MUGALU washabiki wa Tanzania ni pasua kichwa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ww upo shabiki was simba gani huekewi hata Nini kiniaendelea sc , mgogoro was kagere na kocha upo na ataondoka TU kwa tarifa yako

      Delete
  5. Na Kahata nae ana bifu nae maana naye hachezi siku hizi, vp kuhusu Bwalya naye anataka kuondoka Simba si ndio hivyo yani mchezaji asipochezeshwa tu shida huyo Kagere amecheheza mechi za ligi karibu 7 na ana magoli manne kocha alikuwa analaizmishwa kumchezesha acheni unafki washabiki wa simba mnafanya watu mpaka waandike makala ndeeeeeeeeeeeeeefu

    ReplyDelete
  6. Nan kawaambia kocha ana bifu na Kagere?ndan y tz Kuna waandishi wengi uchwara wafuasi wa simba na yanga kazi yao kutumika na izo tim kama alivyo uyu mwandishi wa hi blog mfuatilie vizuri anaichonganisha Simba mno iwe kwa viongozi na mashabiki au viongozi kwa viongozi bahat nzuli viongozi wa simba wanamjua wanampotezea t.Kagere awe na bifu na kocha kisa hachezi je Kahata.Ndemla.Ajib.Gadiel.Sheva.Morison n.k wote hao ana bifu nao?kila kocha Dunian ana machaguo kutokana na mfumo wake sisi tutamuhukumu kocha kwa matokeo t hutaki bac lkn huo ndo ukweli

    ReplyDelete
  7. Mimi inanishangaza Sana kila mmoja angepewa dk 45 Kati yake,Boko Na Mugalu lakini Kocha anamng'ang'ania Boko Tu,hii issue ya kuchezesha mshambuliaji mmoja hasa mechi za nyumbani haivutii kabisa,team inashindwa kupata ushindi nyumbani hii aibu hata Kama Ni hesabu za kufuzu,ugenini .inaweza kuwa sawa lakini nyumbani siafiki.

    ReplyDelete
  8. ha ha ha ha ha nyie mikia fc vp mpeni hela zake huyo babu kagere

    ReplyDelete
  9. Mpeni hela zake jamani acheni kuwasumbua wazee hao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ukiazi ww fuatilia team yako Chandimu mchangani huko, usimshobokee hovyo babaako.
      Babaako abakufanyia mpango mwanaeakuingize kimataifa maana huna uwezo wakujiingiza mwenyewe ukashiriki

      Delete
  10. Kiukwk mm binafsi simpendi huyo kocha basi tu!! Ningekuwa namiliki hiyo timu namfukza huyo kazi mara moja!!!

    ReplyDelete
  11. Harud uchebe aseee maana hapa tutakufa na presha

    ReplyDelete
  12. Huu mnaoleta washabiki wa simba ni uzwazwa uliopitiliza mbona alivyoshinda NIGERIA hamkuongea yote ndio shida ya kushabikia mpira ukubwani na kwenye mitandaio ya kijamii. Yani timu imevuka around ya kwanza tena dhidi ya timu kutoka Nigeria mtu ananalamika kweli chizi sio mpaka aokote maokopo

    ReplyDelete
  13. Sc mnaweza bill chama mnaweza kutuletea balaa jipya la mwaka mpya 2021 , kwa Simba hii 🤗🤗🤗 kiukweli mnaweza kutuletea aibu kubwa zaidi ya mwaka Jana na kocha uchebe 🤠🤠🤠

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic