October 24, 2015


Baadhi ya wafuaaji wa Ukawa wamevamia katika makao makuu ya Yanga na kutaka kuchana bendera zilizokuwa zimetundikwa.


Makao makuu ya Yanga mitaa ya Twiga na Jangwani ilikuwa imepambwa kwa bendera za CCM.

Wafuasi hao wa Ukawa walikuwa wanatoka kwenye mkutano wa kufunga kampeni kwenye Viwanja vya Jangwani walionyesha kuchukizwa na bendera hizo na kutaka kuzichana huku wakitishia kufanya vurugu.

Hali hiyo ilisababisha polisi kuingilia na kutuliza hali hiyo huku wakisisitiza kama wangeendelea kufanya vurugu basi wangeanza kutembeza virungu.


Baadhi walionekana kuwa na jazba, wakaendelea kutukana matusi wakiwalaani wanaopenda CCM kuweka bendera za chama wanachokiunga mkono huku wakiwa wamesahau ni klabu ya watu wote hata wasiopenda CCM.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic