MISHETTO AKIWA KAZINI... |
Mtanzania Charles
Mishetto ameonyesha hataki utani baada ya kupata namba katika kikosi cha kwanza
cha kikosi cha Rabestein FC.
Rabestein FC inashiriki
daraja la nne na Mishetto sasa ni kati ya wachezaji tegemeo. Ndiyo maana
amekuwa akijifua vilivyo kuhakikisha yuko fiti kila idara.
Mishetto aliwahi kuichezea Stand United kabla ya kwenda Ujerumani ambako amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na huu ukiwa ni msimu wa kwanza.
“Kweli nimepania kufanya vizuri na haiwezi kuwa lahisi, lazima nijitume na kujiweka vizuri kimwili pia,” alisema Mishetto.
0 COMMENTS:
Post a Comment