November 12, 2015


Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto leo alilazimika kufanya kazi ya ziada kuwatoa nje waandishi wa habari kutoka Algeria.


Waandishi hao waliingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Taifa Stars chini ya Charles Boniface Mkwasa ikiendelea na mazoezi.

Kizuguto aliwataka kutoka uwanjani, akawakataza kurekodi na akatoa ruhusa ya wao kurejea baada ya mazoezi kwa ajili ya kuwahoji makocha na wachezaji.

Ingawa walionyesha ubishi, msimamo wa Kizuguto uliwafanya washindwe kuendelea kulazimisha na kweli wakatoka nje.

Stars inavaa Algeria keshokutwa Jumamosi katika mchezo wa kuwania kucheza Kombe la Dunia.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic