November 12, 2015

MARHEZ (KUSHOTO) MARA BAADA YA KUWASILI NA KIKOSI CHA ALGERIA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.

Kikosi cha Algeria kimetua nchini tayari kwa mechi ya keshokutwa dhidi ya Taifa Stars lakini Waarabu hao wamekataa katakata kuzungumza na waandishi wa habari.


Pamoja na kusheheni mastaa kadhaa, ndani ya kikosi hicho kuna wachezaji wanaocheza England wakiwemo Nabil Bentaleb na Riyad Marhez.
 
MARHEZ AKIITUMIKIA LEICESTER CITY Bentaleb anakipiga Tottenham Hotspur ya England na ameingia nayo mkataba hadi mwaka 2020.
 
BENTALEB
Kiungo huyo tayari ameichezea Spurs mechi 45 ingawa hajafunga bao hata moja, ameicheza Algeria mechi 17 na kufunga mabao matatu.

 Marhez ameichezea Lecester City mechi 60 tokea mwaka 2014 na tayari amefunga mabao 14.
Wote hao wamegoma kuzungumza na waandishi wa habari.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic