Utaona katika kikosi cha Barcelona kuna kitu
kimeongezeka tokea Luis Enrique aanze kazi.
Sasa inaonekana ni timu isiyoshikika, ngumu kuzuilika
na haonekani wa kuizuia.
Lakini kama utapiga hesabu nzuri, unaona Bayern Munich
chini ya Pep Guardiola inaweza kufanya hivyo, maana nayo ni kiwembe.
Zikiingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, basi
huenda ikawa fainali tamu kuliko zikikutana timu nyingine au moja kati ya hizo
na timu nyingine.
Barcelona imeitandika AS Roma kwa mabao 6-1 nyumbani
kwao, lakini unajua namba mziki wa wakali kama Arjen Robben, Tomas Muller, Robert
Lewandowski, Douglas Costa na Kingsley Coman ulivyo mgumu kuzuilika.
Kama timu hizo zitakutana fainali, kila mmoja
atafurahia kuitazama fainali hiyo, maana itakuwa burudani ya aina yake.
Kwa mwenendo wa timu hizo kwa sasa, kila moja inaweza
kufika fainali. Je, hazitakutana katikati? Ikiwa hivyo, itakuwa burudani bomba
ya mwisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment