Kipa wa Yanga,
Deo Munish maarufu kama Dida amekuwa akijifua vilivyo akionyesha amepania hasa
kurejea katika kikosi cha kwana.
Dida anajua
kama atarejea katika kikosi cha kwanza, basi ana nafasi ya kucheza pia katika
timu ya Tanzania Bara, Kili Stars au ile ya taifa, Taifa Stars.
Dida hana
nafasi katika kikosi cha Yanga, Kili Stars au Taifa Stars ambazo aliwahi
kuzichezea. Kwa sasa nafasi katika viko vyote viwili vya taifa ziko chini ya Aishi Manula na Ally Mustapha ambaye ndiye kipa namba moja wa Yanga.
Katika mazoezi
ya Yanga, kipa huyo alikuwa akijifua kwa juhudi kubwa.
Pamoja na
mazoezi mengine, alikuwa akiitumia nguzo ya goli kama sehemu ya mazoezi ili
kuongeza wepesi wa mwili na kuufanya kuwa unaonyumbulika ambalo ni jambo jema
kwa kipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment