Mwenyekiti wa Kamati Taifa Stars, Farough Baghozah
amewashukuru watanzania kwa michango yao waliyoitoa kuispaoti timu ya Taifa
‘Taifa Stars’ katika michezo ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018 nchini
Urusi dhidi ya Algeria.
Farough alianza kwa kuwashukuru watanzania kwa
kujitokeza kwa wingi katika mechi ya Taifa Stars na Algeria na kuwashukuru pia
wale wote waliosafiri na timu hiyo ya Taifa, Taifa Stars kwenda Algeria katika
mechi ya marudiano.
Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo kuishukuru
Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Makamu wa Raisi Mama Samiha
Suluhu, Raisi Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani
na viongozi wote wa chama na serikali kwa njia moja au nyingine katika kusapoti
timu ya Taifa Taifa Stars kwenye Mchezo na Algeria
Naye Mkuu wa mkoa Dar es salaa, ambaye ni mlezi wa
kamati hiyo, Mh Mecky Sadick aliwashukuru watu wote, kuanzia wanakamati kwa
jinsi walivyojitoa kwa muda wao wote katika maandalizi na hasa kuhamasisha
watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao ya taifa kwa
kuomnyesha uzalendo.
Kwa namna ya kipekee Mecky Sadick amewashukuru watu
wote na makampuni yaliyojitokeza katika kuchangia Timu ya taifa wakiwemo
Jubilee Insurance, Equity Bank, PPF, Serena Hotel, GSM, bila kusahau vyombo
vote vya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine waliweza kujitoa na
kuhamasisha watanzania wajitokeze kwa wingi uwanja wa taifa kuishangilia timu
yao.
Katika mchakato mzima wa awali wa mechi ya kufuzu
kombe la dunia 2018, Kamati kupitia kwa wadau mbalimbali iliweza kuchangisha
pesa jumla ya milioni 122,640,000 za kitanzania, dola za kimarekani 19,800 na
177,000 kutoka tigo pesa na airtel money.
Matumizi ni dola za kimarekani 70355, na milioni
47,904, 743 za kitanzania.
Mwisho kamati imewashukuru sana Watanzania na na
kuwaomba wadumishe umoja wtue.. Nchi Yangu, Timu Yangu Taifa langu.
0 COMMENTS:
Post a Comment