Rais wa Chama cha Soka cha Sudan (SFA), Dk
Jaffar Mutasim, amechaguliwa kuwa rais mpya wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika
Mashariki na Kati (Cecafa), jana akichukua nafasi ya Leodegar Tenga wa
Tanzania.
Mutasim
amechaguliwa kuchukua nafasi hiyo kutoka kwa Tenga ambaye alikaa madarakani
tangu mwaka 2007. Tenga ameongoza Cecafa kwa vipindi viwili vya miaka
minne-minne.
Katika
uchaguzi uliofanyika jana jijini hapa, Mutasim alipata kura sita kati ya 10
zilizopigwa na kuwapiku wapinzani wake Mganda, Lawrence Mulindwa aliyepata tatu
na Mrwanda Vincent Nzamwita (1) na Juneid Bashar Tilmo wa Ethiopia aliyejitoa.
Baada
ya matokeo hayo, Mutasim aliwashukuru wajumbe waliomchagua na kwamba
atahakikisha anapigania mchezo huo uweze kusonga mbele.
Viongozi mbalimbali wa soka wakiwemo wale wa
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), walihudhuria uchaguzi huo akiwemo
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Robert Asembo.
0 COMMENTS:
Post a Comment