November 26, 2015

Beki wa zamani wa Simba, Ramadhani Wasso amerejea uwanjani na sasa anakipiga katika timu ya Panone inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.


Wasso anakipiga katika timu hiyo ya mjini Moshi na leo ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Wasso raia wa Burundi alikuwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wanajifua.

Wasso anaamini bado yuko fiti na si mzee anayeweza kushindwa kufanya yake kama ambavyo wengi wanaamini.

Beki huyo mahiri wa kushoto, pia aliwahi kukipiga Yanga aliyojiunga nayo akitokea Simba ambako aliaga anakwenda kufanya majaribio nchini Ubelgiji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic