KAVUMBAGU ANAYEKIPIGA AZAM FC, LEO AMEICHEZEA BURUNDI IKILALA DHIDI YA DR CONGO |
Pamoja na Amissi Tambwe na Didier Kavumbagu kuingia katika kipindi
cha pili wakati Burundi ikiivaa DR Congo, wameshindwa kuikomboa.
Burundi imefanikiwa kupata sare ya mabao 2-2 ikiwa ugenini katika
mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia nchini Russia.
Kavumbagu aliingia kuchukua nafasi ya Selemani Ndikumana aliyewahi kuichezea Simba huku Tambwe akiingikia kuchukua nafasi ya Gael Bigirimana.
Katika mechi ya kwanza, Burundi ililala kwa mabao 3-2 ikiwa
nyumbani Bujumbura. Hivyo sare hiyo maana yake imeng’olewa kwa jumla ya mabao
6-5.
Katika mechi ya kwanza, Tambwe anayekipiga Yanga na Kavumbagu
kutoka Azam FC, walimaliza dakika 90 wakiwa benchi.
Baada ya mechi hiyo, wachezaji hao wanalazimika kurejea nchini
mapema na kuelekeza nguvu zao katika Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment