Kiungo
mshambuliaji, Brian Majegwa amesema angependa kuondoka Azam FC.
Majegwa
amesema Azam FC haikumtendea haki kwa mambo mengi, hivyo bora aangalie
utaratibu mwingine kistaarabu.
Majegwa
raia wa Uganda kwa sasa anafanya mazoezi na Simba ambayo ameiandikia barua
kuomba apewe nafasi ya kufanya mazoezi.
“Ninafurahia
kuona Simba wamekuwa waelewa na kunipa nafasi ya kufanya nao mazoezi.
“Pia
ninasikia faraja kuona watu wanaweza kukubali ombi lako wakiamini unataka
kukilinda kipaji chako,” alisema Majegwa.
“Lakini
kwangu ni wakati mwafaka wa kuondoka Azam FC, nina mengi ya kusema kwa nini
nitafanya hivyo, lakini si sasa,” alisema.
Majegwa
alipekwa kwa mkopo KCCA baada ya kuonekana Kocha Stewart Hall hakuwa
akifurahishwa na kiwango chake, jambo ambalo Mganda huyo, hakulifurahia.
0 COMMENTS:
Post a Comment