November 30, 2015


Mganda Brian Majegwa sasa ni mali ya Simba na atakuwa katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.


Simba imefikia makubaliano na Azam FC ili kumtwaa Majegwa raia wa Uganda, akipige Msimbazi.

Makubaliano hamefikiwa baada ya kikao kizito kilichofanyika jijini Dar es Salaam jioni hii na Simba na Azam FC kufikia mwafaka kuhusiana na Majegwa.

Bado kila upande umekuwa ukifanya siri, lakini taarifa zinaeleza kwamba Mganda huyo ameishapewa taarifa na sasa kinachofuatia ni kumalizana kwa kila upande kwa vitendo.

Majegwa alirejea nchini na kuomba kufanya mazoezi na Simba ili kulinda kiwango chake.


Lakini Azam FC ilianza kulalamika kwamba ni mchezaji wao lakini bado Majengwa aliweka msimamo kwamba angependa kucheza Simba na Azam FC wamwache.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic