November 30, 2015



Kiungo Andrey Coutinho yuko jijini Dar es Salaam, lakini uongozi wa Yanga, umepitisha uamuzi wa kumtema.


Uamuzi wa Yanga umepitishwa baada ya majadiliano kati ya uongozi na benchi la ufundi kukubaliana.

Habari zinaeleza Yanga iko katika hatua za kufikia makubaliano na Coutinho ili kuvunja mkataba wake.
Kocha Hans van der Pluijm ameridhia kuachana na Coutinho kwa kuwa amekuwa hana msaada wa kutosha.


Lakini Yanga kwa sasa inafanya mchakato huo, kama pande mbili zitashindwa kufikia mwafaka, basi raia huyo wa Brazil ataendelea kubaki Yanga hadi mkataba wake utakapokwisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic