November 28, 2015


Mshambuliaji Elias Maguri amebakiza miezi sita tu katika mkataba wake na Stand United, sasa timu yake inapambana kuhakikisha inamuuza ndani ya muda huo ili asiondoke kama mchezaji huru.


Awali, Stand United baada ya kusikia habari za Maguri kutakiwa na TP Mazembe, ikakubali kumuuza kwa dola 50,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 100, lakini bado kuna kitu kinawachanganya.

Ofisa Habari wa Stand United, Deo Kaji Makomba, amesema wameona  wakizubaa Maguri mwenye mabao tisa katika Ligi Kuu Bara, anaweza kuondoka bure, hivyo wanatafuta namna ya kuzipata fedha za usajili wake.

“Tulimsajili Maguri kwa mkataba wa mwaka mmoja, hivyo baada ya msimu huu atakuwa amemaliza majukumu yake ya kuitumikia timu yetu na atakuwa huru.

“Tunaangalia jinsi gani ya kufanya ili tuweze kufaidika naye, kwani hata sisi bado tunahitaji huduma yake, kama itashindikana basi tumuombee kwa Mungu mipango yake ya kwenda Mazembe ikae sawa katika kipindi hiki ambacho bado ana mkataba ili na sisi tuweze kufaidika naye,” alisema Makomba.


TP Mazembe ambayo imetuma maofisa wake Ethiopia kumtazama Maguri akiichezea Kilimanjaro Stars katika Kombe la Chalenji, inataka kumsajili straika huyo ili kuziba pengo la Mbwana Samatta anayeondoka klabuni hapo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic