HOTELI YA SERENA |
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars’ imerejea jana jioni ikitokea chini Afrika Kusini
ilipokuwa imeweka kambi ya siku kumi, ambapo leo jioni itafanya mazoezi katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mzalendo Charles
Boniface Mkwasa, kimefikia katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta, na
leo jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Washambuliaji
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR
wameungana kambini na wachezaji wenzao jana na kufanya kikosi cha Stars
kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.
Wapinzani
wa Taifa Stars, timu ya Taifa ya Algeria wanatarajiwa kuwasili leo saa 12 jioni
nchini kwa usafiri wa ndege binafsi, na kufikia katika hoteli ya Kilimanjaro
Kempsink (Hyatt) ambapo kesho jioni Ijumaa watafanya mazoezi katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es slaam.
Wakati
huo huo waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Mali, mwamuzi wa kati Keita
Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na mwamuzi wa akiba Coulibaly
Harouna tayari wameshawasili nchini leo asubuhi, huku mtathimini wa waamuzi
Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger alishawasili nchini tangu juzi
usiku.
Kamisaa
wa mchezo huo Mukuna Wilfred kutoka nchini Zimbambwe anawasili nchini leo
mchana kwa shirika la ndege la Afrika Kusini (South Africa Airways
0 COMMENTS:
Post a Comment