November 12, 2015


Jina la Rais John magufuli na lile la mshambuliaji wa Stand United, Elius Maguli linaonekana kuwatatiza baadhi ya wanamichezo.


Mmoja wao ni mtangazaji wa EFM, Maulid Kitenge ambaye alilazimika kujitengeneza mara kadhaa kutokana na kusema Maguli badala ya Magufuli au Maguli badala ya Magufuli wakati akiripoti kutoka nchini Afrika Kusini.

“Haya majina yanababaisha kidogo,” alisema Kitenge ambaye pia ni mchambuzi wa gazeti la Championi.


Pamoja na Kitenge, wanamichezo kadhaa wamekuwa wakiyachanganya majina hayo wakati wa kuandika na kuzungumza.

Magufuli amekuwa gumzo kutokana na ziara zake za kushitukiza ambazo zimewavutia sana Watanzania wengi wanaopenda watu wachape kazi.

Lakini Maguli ndiye mchezaji anayeongoza kwa kupachika mabao mengi akiwa na kikosi chake cha Stand United katika Ligi Kuu Bara. Huenda ndiyo maana wote ni gumzo kipindi hiki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic