Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na
mzabuni wa tenda ya elektroniki benki ya CRDB, leo limetangaza tenda ya kumsaka
mshauri wa mfumo wa Elektroniki (Consultant) kwa ajili ya kupitia
mapungufu yaliyopo katika mfumo wa uuzaji tiketi wa elektroniki katika michezo
ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
TFF imetangaza tenda hiyo ili kumpata mshauri wa mfumo huo wa
tiketi za elektroniki, ambao ulisamishwa na serikali mapema mwaka huu mwezi
Aprili.
Maombi
ya tenda yawasilishwe katika ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF zilizopo Karume jijini
Dar es salaam, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 10 jioni siku za kazi Jumatatu
mpaka Ijumaa.
Gharama
ya fomu ya kuombea tenda ni shilingi laki moja (100,000), na mwisho wa maombi
ni Disemba 17, 2015.
0 COMMENTS:
Post a Comment