November 13, 2015

MUSONYE

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamau za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Theresia Musonye kilichotokea leo asubuhi katika mji wa Kakamega nchini Kenya.

Katika salamu zake, Malinzi amempa pole Musonye na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu na watanzania wote, wako pamoja nae katika kipindi hiki cha kigumu cha maombelezo na kuwapa pole ndugu,jamaa na wafiwa wote.
Bi Theresia Musonye amefariki akiwa na umri wa miaka 77, taarifa zaidi na taratibu za mazishi zitatolewa na familia ya marehemu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic