November 12, 2015


 
BOSSOU (KUSHOTO) AKIWA KATIKA BENCHI LA YANGA, KABLA YA KWENDA TOGO KUICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA....

Uganda wameonyesha inawezekana baada ya kuitwanga Togo kwa bao 1-0 katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia mjini Lome.

Shujaa wa Uganda ni Farouk Miya aliyefunga bao pekee katika dakika ya 39 na kuizamisha Togo ikiwa nyumbani.

Kilichovutia ni kwamba makocha wawili, Sredojevich Milutin ‘Micho’ wa Uganda na Tom Saintfiet wa Togo wote waliwahi kuinoa timu kongwe ya Yanga kwa nyakati tofauti.

Lakini vitu vingine viwili katika mechi hiyo viliihusu soka ya Tanzania ni kuumia kwa Hamisi Kiiza wa Simba ambaye alitolewa na nafasi yake ikachukuliwa na straika wa zamani wa Azam FC, Bryan Umonyi.


Pia beki Vicent Bossou wa Yanga, naye aliendelea kubaki benchi kwa dakika zote 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic