November 12, 2015

 
TAMBWE

DRC imefunga Burundi kwa mabao 3-2 ikiwa nyumbani Bujumbura katika mechi ya kuwania kucheza Kombe la Dunia.


Wakati Burundi inapoteza, washambuliaji wawili wanaong’ara Tanzania, Amissi Tambwe wa Yanga na Didier Kavumbagu wa Azam FC walikuwa benchi kwa dakika zote 90.

Mbali na hao, Laudit Mavugo anayeonekana kufukuziwa na Simba kwa juhudi, naye alikuwa benchi kwa dakika zote 90.
 
MAVUGO
Badala yake, Burundi ikawatumia Selemani Ndikumana aliyewahi kucheza Simba na Cedric Amissi aliyefunga mabao yote mawili ya Burunfi hiyo leo.

DR Congo walitangulia kupata bao kupitria Yannick Bolasie kabla ya Cedric kusawazisha na timu zikaenda mapumziko 1-1.


Kipindi cha pili, dakika ya 83, Cedric akatupia la pili lakini Firmin Mubele Ndombe aliyeingia kipindi cha pili akafunga mabao mawili katika dakika ya 86 na 88 na kuimaliza Burundi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic