Kikosi cha Zanzibar Heroes kinachoongozwa na nahodha
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kimeng’olewa katika michuano ya Chalenji inayoendelea
nchini Wethiopia.
Zanzibar Heroes imefungwa mabao 4-0 na Uganda na kuwa
kipigo chake cha pili baada ya kuanza michuano hiyo kwa kufungwa bao 1-0 na
Burundi.
Kwa kipigo hicho, maana yake Zanzibar Heroes haina
nafasi ya kusonga mbele kutoka Kundi B.
Mechi ya mwisho watakutana na Kenya ambao walianza
michuano hiyo kwa kuituliza Uganda kwa kuichapa mabao.
Katika mechi ya leo, Zanzibar walionekana hawana nguvu
kabisa ya mipango na muda mwingi The Cranes walitawala mchezo.
The Cranes chini ya Sredojevic Milutin ‘Micho’
wangeweza kushinda zaidi ya mabao hayo kama wangekuwa makini katika umaliziaji.
0 COMMENTS:
Post a Comment