Katika hali iliyozua sintofahamu, mlinzi wa
getini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wikiendi iliyopita alijikuta akimshushia
kipigo mwamuzi wa kike kabla ya mechi ya Ligi Daraja la Pili kati ya Pamba na
Bulyanhulu FC.
Mwamuzi huyo, Martha Joshua ambaye siku hiyo
alipewa majukumu ya kuwa mwamuzi wa akiba katika mchezo huo, alizuiwa kuingia
uwanjani na mlinzi huyo ambaye jina lake halikufahamika hali ambayo ilizua
mtafaruku.
Filamu kamili ilikuwa hivi; Martha akiwa na
waamuzi wenzake akiwemo Daniel Warioba, walifika getini hapo na kujitambulisha,
wawili wakaruhusiwa kuingia lakini Martha licha ya kuonyesha vielelezo vyote
vya wasifu wake bado mlinzi huyo aliweka ngumu akimtaka alipe kiingilio ndipo
akalazimisha kuingia.
Wakati Martha akiingia kulikuwa na majibizano
makali, ndipo ghafla makofi yakatembea kwa wawili hao na kusababisha mvutano na
vurugu iliyodumu kwa dakika kadhaa kabda ya kuamuliwa na Martha kuingia ndani.
Alipoulizwa Mwenyekiti wa Waamuzi Mkoa wa Mwanza,
Jumanne Shengelo, alisema: “Yawezekana
wana visa vyao hao, sisi hatujapata ripoti hiyo.” Alipoulizwa Martha alisema:
“Sikupeleka ripoti kwa kuwa mlinzi hakuwa muungwana, nikaamua kuachana naye.”
0 COMMENTS:
Post a Comment