Nahodha na beki wa kati wa Taifa Stars, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’, ametangaza rasmi kuwa, atastaafu kuichezea timu hiyo miaka
mitatu ijayo.
Kauli huyo, aliitoa jana Alhamisi mara baada ya kumalizika
kwa mazoezi ya timu yake ya Yanga kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini Dar.
Mara baada ya Stars kufungwa na Algeria mabao
7-0, kuliibuka maneno kuwa Cannavaro na beki mwenzake wa kati, Kelvin Yondani,
wanaonekana kuchoka kutokana na umri kuwatupa mkono.
Cannavaro ameliambia gazeti hili kuwa umri wake
siyo mkubwa kiasi cha yeye kustaafu kuichezea Stars.
“Hizo kejeli na maneno ya watu nimeyazoea muda
mrefu sana, kuhusiana na kiwango changu kushuka na umri kuwa mkubwa, hivyo
ninachofanya ni kunyamaza tu.
“Muda wa kustaafu bado haujafika, nitafikiria
hivyo miaka mitatu ijayo na tena nikistaafu hapo nitaendelea kuichezea Yanga,
ikitokea nimeondoka Yanga basi jua kuwa ndiyo mwisho wangu wa soka umefika kwa
sababu sifikirii kuichezea klabu nyingine mara baada ya hapo,” alisema
Cannavaro ambaye ni nahodha wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment