December 3, 2015

KOCHA MKUU WA VALENCIA, GARRY NEVILLE (KULIA) AKIWA NA MSAIDIZI WAKE NA MDOGO WAKE, PHIL NEVILLE.

Klabu ya Valencia ya Hispania imetoa kali ya mwaka baada ya kumtangaza Kocha msaidizi wa England, Gary Neville kuwa kocha wake mkuu.



Gary anaungana na mdogo wake Phil Neville ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Valencia tokea Julai, mwaka huu.
 
Tayari Garry ameaga katika runinga ya Sky Sports ambayo ilikuwa na mkataba naye akiwa mchambuzi.

Neville wote wawili walikuwa wachezaji tegemeo wa Manchester United chini ya Kocha Alex Ferguson.

Pia ni kati ya wachezaji wachache ambao walipata mafanikio makubwa wakiwa na Manchester United.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic