December 3, 2015


Wachezaji makinda pia watapata nafasi kubwa ya kuunganishwa katika kikosi cha kwanza.


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr amesema wachezaji vijana wamekuwa wakionyesha juhudi kubwa mazoezini.

“Tumekuwa tukichanganyika na wachezaji vijana, wako ambao wanaonyesha juhudi kubwa na kweli wana uwezo.

“Lakini wanahitaji muda zaidi wa mafunzo, pia wanatakiwa kuwa na nidhamu ya kutaka kufanikiwa,” alisema.

“Lazima tutawapa nafasi zaidi kama ambavyo unaona wanafanya mazoezi pamoja na wachezaji wa timu kubwa. Watakaofanya vizuri, nafasi kwao itaongezeka.”


Simba inaendelea na mazoezi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara ambayo ilisimama na sasa inatarajiwa kuendelea Desemba 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic