December 28, 2015

EVANS AVEVA

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema suala la kuibinafsisha klabu hiyo linahitaji ungalifu mkubwa katika mambo kadhaa.

Aveva amesema kuwa Simba inaweza kubinafsishwa lakini lazima uongozi uhakikishe na kujua thamani ya klabu  hiyo ikiwa imeishajiridhisha kama ubinafsishaji kweli una faida.

“Ni suala la kitaalamu, lazima kuliangalia na kutathmini. Kama tutapata uhakika basi ni suala la thamani ya klabu ya Simba. Hapa si kuangalia majengo, sijui magari na uwanja ambao tunataka tuanze kuujenga.

“Lakini kuna suala la maana ya thamani ya Simba kama klabu, hili linahitaji wataalamu waliotulia na kufanya tathmini ya uhakika. Baada ya hapo, litafuatia suala la wanachama kuelimishwa kuwa nini kinafanyika, zipi faida zake.

“Wanachama ndiyo wamiliki wa klabu, lazima waelimishwe na baada ya hapo kuna suala la katiba ambayo inasema wamiliki wa Simba ni wanachama. Ukiangalia hapa utaona hili si jambo dogo,” alisema Aveva.

Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu kama Mo alikuwa ameeleza wazi nia yake ya kutaka kuinunua Simba kwa asilimia 51 na zilizobaki 49 zitaachwa kwa wanachama wengine wa Simba. Lakini uongozi wa Simba umekuwa ukisema unalisikia suala hilo kwenye vyombo vya habari tu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic