December 1, 2015


TP Mazembe ndiyo wawakilishi wa Afrika katika michuano ya ubingwa wa dunia upande wa klabu.

Michuano hiyo inaanza Desemba 10 na TP Mazembe inatakiwa kucheza mechi tatu kabla ya kufika fainali.

Desemba 10 itacheza Auckland City, ikishinda itakutana na timu nyingine iliyovuka na kama itashinda tena itaingia nusu fainali.

Mechi ya nusu fainali itakutana kati ya timu ambayo haijajulikana au River Plate ya Argentina na wakishinda hiyo basi ni fainali.

Lionel Messi atakuwa na Barcelona ambayo inaanzia moja kwa moja hatua ya nusu fainali kwa kucheza na mshindi kati ya America dhidi ya Guangzhou Evergrande ya China.

Iwapo Mazembe itashinda mechi hizo tatu, Barcelona ikashinda hiyo moja, basi nyota zaidi katika timu zitakazocheza fainali itakuwa ni Messi na Samatta kutoka Tanzania.

Hata hivyo Mazembe wanalazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanashinda mechi hizo tatu kabla ya kuikamata Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic