December 29, 2015


Mshambuliaji nyota wa Yanga, Donald Ngoma amelazimika kusafiri kwa dharura kwenye nchini Afrika Kusini, kumkomboa mwanaye.

Mwanaye Ngoma ameshikiliwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo jijini Afrika Kusini baada ya kuonekana kuna tatizo katika pasi yake ya kusafiria.

Mkewe Ngoma na mwanaye walikuwa safarini kuja nchini kwa ajili ya kuungana na Ngoma kabla ya tatizo hilo kutokea na maofisa wa uhamiaji wa Afrika Kusini wakata kupatikana cheti cha kuzaliwa cha mtoto huyo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amethibitisha kutokea kwa tatizo hilo na Yanga imempa Ngoma ruhusa.

“Kweli amesafiri, atakuwa huko kwa muda akishughulikia tatizo hilo baada ya hapo ataungana na wenzake,” alisema.


Ngoma raia wa Zimbabwe amekuwa chachu katika safu ya ushambulizi ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic