December 10, 2015


Mabingwa wa Afrika, TP Mazembe sasa wamejua mpinzani wao wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia kwa klabu.


Mazembe inakutana na Sanfrecce Hiroshima ya Japan ambayo leo imeanza michuano hiyo vizuri kwa kuichapa Auckland City ya New Zealand.

Mabao mawili ya Minagawa na Shotani, yalitosha kuwapa ushindi wenyeji hao na sasa wanakutana na TP Mazembe Jumapili.

Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanatarajia kuongoza mashabulizi ya Mazembe ambayo tayari ipo mjini Osaka kwa ajili ya mechi ya Jumapili.


Kiutaratibu wa michuano hiyo, TP Mazembe imepewa nafasi ya kuanzia robo fainali, ikishinda mechi ya Jumapili, itacheza nusu fainali desemba 16 dhidi ya River Plate ya Argentina, ikishinda, basi ndiyo fainali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic