Blogu hii ilikuwa ya kwanza jana kukuandikia mshambuliaji Paul Kiongera amejiunga tena na Simba iliyoko mjini Zanzibar kwa ajili ya kambi.
Tayari mshambuliaji huyo Mkenya,
ameanza rasmi mazoezi pamoja na wenzake kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Kiongera amerejea Simba baada ya
kucheza KCB ya Kenya mkopo, Simba ilimpeleka huko baada ya kuwa ameumia na
kuanza matibabu nchini India ambayo yaligharimiwa na klabu hiyo kutoka eneo la
Kariakoo.
Sasa Kiongera amerejea ili kuongeza
nguvu katika safu ya ushambuliaji ambayo imeonekana kusuasua.
0 COMMENTS:
Post a Comment