Mechi mbili tu,
zinawatosha Watanzania Mbwana Samatta kuweka rekodi ya kucheza fainali ya Kombe
la Dunia kwa klabu.
Kwa Mujibu wa
ratiba ya michuano hiyo ya Fifa ya Kombe la Dunia kwa Klabu, Mazembe imepangwa
kuanzia katika hatua ya robo fainali huku Barcelona ikipewa heshima ya kuanzia
nusu fainali.
Tayari Mbwana
Samatta na Thomas Ulimwengu wamekanyaga ardhi ya Japan wakiwa na kikosi cha cha
TP Mazembe kutoka DR Congo.
TP Mazembe
ambao ni mabingwa Afrika, watacheza mechi yao ya kwanza Desemba 13 dhidi ya mshindi
wa mechi ya kwanza kati ya wenyeji Sanfrence Hiroshima ya Japan dhidi ya
Auckland City ya New Zealand.
Iwapo Mazembe
itashinda mechi yake hiyo ya kwanza, moja kwa moja inakwenda kukutana na
mabingwa wa America Kusini ambao ni River Plate ya Argentina na mechi itapigwa
Desemba 16, hiyo itakuwa ni nusu fainali ya kwanza.
Nusu fainali ya
pili, itazikutanisha Barcelona dhidi ya
mshindi wa mechi kati ya America ya Mexico dhidi ya Guangzhou Evergrande ya
China.
Iwapo Mazembe
itashinda katika nusu fainali ya kwanza, Barcelona ikashinda nusu fainali ya
pili, basi timu hizo zitakutana katika fainali itakayopigwa Desemba 20.
0 COMMENTS:
Post a Comment