NDEMLA... |
Wachezaji wa Simba waliokuwa katika kambi ya timu ya
Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wameungana na wenzake mjini Zanzibar.
Simba imeweka kambi mjini Zanzibar kujiandaa na Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuendelea Desemba 12 na itaanza kazi na Azam FC.
Said Ndemla, Hassan Isihaka na Mohamed Hussein
‘Tshabalala’ ndiyo wachezaji waliokuwa katika katika kikosi cha Tanzania Bara
kilichoshiriki michuano ya Chalenji na kutolewa katika hatua ya robo fainali.
Ibrahim Ajibu
tayari alijiunga na kikosi cha Simba mapema kwa kuwa hakwenda Ethiopia
ilipofanyika michuano ya Chalenji baada ya timu kuondoka na kumuacha.
Awali hakupewa maelezo, lakini baadaye akatakiwa
kwenda Ethiopia, lakini akaueleza uongozi wa TFF hakuwa jijini Dar es Salaam.
Kuungana kwa wachezaji hao, maana yake Simba ina
kikosi chake kamili kasoro Waganda wawili, Hamisi Kiiza na Juuko Murishid.
0 COMMENTS:
Post a Comment