Si unamjua yule
binti mkali wa kupiga danadana na kuuchezea mpira, sasa yuko taabani hospitali
ya Mwanyamala.
Anaitwa Hadhara
Charles, ameungua mgongoni, mikono pia baada ya kumwagiwa maji na mtu aliyeitwa
ni mke wa mjomba wake.
Hadhara
amesema: “Kulitokea mzozo, wakanitaka nihame. Wakati naondoka mke wa mjomba
wangu akanimwagia maji ya moto mgongoni. Ninasikia maumivu makali sana.”
Binti huyo
anaomba msaada na amelazwa katika wodi namba 3 Hospitali ya Mwananyamala jijini
Dar es Salaam.
Hadhara amekuwa maarufu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuuchezea mpira.
0 COMMENTS:
Post a Comment