January 6, 2016


Straika wa Stand United, Elias Maguri, amefunguka kwa kusema kuwa mapumziko ya mara kwa amra katika ligi yanachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha kasi ya wachezaji.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar ambapo kabla ya hapo, ilisimama kwa muda wa mwezi mmoja kupisha timu ya taifa.

Maguri amesema kuwa kwa sasa anajipa tizi la peke yake kwa ajili ya kuimarisha kiwango chake na kudai kuwa mapumziko ya mara kwa mara yanaathiri viwango vyao.

“Mapumziko ya mara kwa mara yanachangia kushusha viwango vyetu kwa kuwa kila mara tunakuwa tunaanza upya, nafikiri hivi siyo vizuri.

 “Kwa upande wangu nimekuwa nikijipa mazoezi binafsi hadi hapo nitakapoungana na timu yangu baada ya mapumziko mafupi ya kuanza maandalizi ya ligi.


“Lengo ni kuhakikisha nafanikiwa kuwa katika kiwango kizuri kuisaidia timu yangu kuweza kumaliza katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi,” alisema Maguri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic