Kipa wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ ambaye kwa sasa anapewa nafasi ya kudaka katika kikosi cha kwanza, amepewa onyo kali na kocha wa makipa wa timu hiyo, Juma Pondamali.
Dida ambaye alikuwa kipa namba moja wa timu hiyo lakini kwa kipindi kirefu amekuwa akisota benchi na kumshuhudia kipa mwenzake, Ally Mustapha ‘Barthez’ akidaka, katika mechi nne mfululizo zilizopita zote ameanza kwenye kikosi cha kwanza.
Pondamali amesema kuwa Dida kwa sasa asijione kama ndiye ana uhakika wa namba kwani anachofanyiwa ni kujaribiwa tu, hivyo kama akionekana anafanya makosa atarudi benchi.
“Dida kumpa nafasi ni sawa na kumpa mtihani tena mgumu, hivyo anatakiwa kuzidi kukaza na asione kama ndiyo ana uhakika, zamani alikuwa ana matatizo ya kufungwa mabao ya mbali, nikamtupa benchi na nikamuagiza amuangalie mwenzake Barthez anavyofanya kwani huwa makini sana golini.
“Hivyo ajue kabisa kipindi hiki kwake ni cha mtihani mzito kupewa nafasi ya kuanza kwenye mechi asijione kama ndiyo amefika kwani nitamtazama kwenye mechi kati ya saba au kumi kama nikiona ana makosa nitamtupa tena benchi,” alisema Pondamali ambaye yupo na timu hiyo kwenye michuano ya Mapinduzi visiwani Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment