January 29, 2016

LYANGA KAZINI....

Straika wa Simba, Daniel Lyanga, amewekewa ulinzi mkali na uongozi wa klabu hiyo ili kumlinda na watu wasiokuwa na nia nzuri na maendeleo yake ya soka pamoja na klabu hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni kuibuka kwa taarifa kuwa mchezaji huyo ameikacha timu hiyo kwa madai kuwa hajamaliziwa madai yake anayodai klabuni hapo.

Kutokana na hali hiyo uongozi wa Simba umeamua kumwekea ulinzi mchezaji huyo ili kuhakikisha havurugwi na watu wasiomtakia mema yeye na klabu kwa jumla.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema Lyanga hana tatizo na klabu bali alikwenda kwao mkoani Kilimanjaro kutokana na masuala ya kifamilia.

“Inatubidi tuwe macho na watu hao wasiomtakia mema mchezaji huyo lakini pia klabu yetu ya Simba ambayo sasa ipo moto kutokana na ufanisi wake mkubwa inaouonyesha uwanjani,” alisema Manara.


Lakini alipopigiwa Lyanga kuhusiana na suala hilo, alisema hakuwa na nafasi kuzungumza wakati huo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic