January 7, 2016


Kocha Stewart Hall ameamua kumpumzisha kipa Aishi Manula na kumpanga mkongwe Ivo Mapunda kuivaa Mafunzo katika mechi muhimu ya Kombe la Mapinduzi.

Azam FC inatakiwa kuishinda Mafunzo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar leo ikiwezekana kwa bao nyingi ili kujiwekea mazingira mazuri kusonga mbele kutoka Kundi B.

Manula alifanya kosa baada ya kuutema mpira uliokuwa mikononi mwaka na kumfikia Vicent Bossou aliyeukwamisha wavuni na kufanya Yanga ipate bao la kusawazisha na matokeo kuwa 1-1 katika mechi iliyopigwa juzi.

Katika kikosi hicho, Hall raia wa Uingereza atawakosa nahodha wake, John Bocco mwenye kadi nyekundu na Didier Kavumbagu ambaye ni mgonjwa.

LEO KIKOSI CHA AZAM FC KIPO HIVI:
1.Ivo Mapunda-3
2.Aboubakar Salum-8
3.Shomari Kapombe-4
4.Erasto Nyoni-6
5.Pascal Wawa-5
6.Abdallah Kheri-25
7.Farid Mussa-17
8.Mudathir Yahaya-20
9.Allan Wanga-9
10.Michael Bolou-29
11.Kipre Tchetche-10

Sub
1.Aishi Manula-28
2.Racine Diouf-21
3.Wazir Salum-26
4.Frank Domayo-18
5.Ramadhan Singano-14
6.David Mwantika-12
7.Ame Ali-24
8.Khamis Mcha-22
9.Said Morad-15

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic