January 8, 2020




Na Saleh Ally
KUMBUKA ule msemo wa “Kila mchukuzi husifu mzigo wake”. Hii ni kawaida kwa kila mwanadamu kupenda kusifia kile anachoamini ni chake.


Wachache sana ambao wana uwezo wa kuzungumzia upungufu wa vile wanavyoamini ni vyao au vile wanavyovimiliki.


Huu ni wakati wa wapenda mpira kuamka, kuanza kukataa mambo ya kipuuzi ambayo yanajitokeza katika mchezo wa soka bila ya kujali anayefanya ni wao au wa wengine.


Unakumbuka tulishadadia kwa pamoja kuhusiana na Kelvin Yondani kumtemea mate beki wa Simba, Asante Kwasi! Bila ya ubishi hakikuwa kitendo cha uungwana na si sahihi kukiunga mkono hata kidogo.


Tulisema bila ya woga licha ya kwamba wako baadhi walijaribu kumtetea Yondani kutaka kuonyesha kama alikuwa akionewa lakini tulisimama katika usahihi na lilikuwa kosa bila ya ubishi.


Huu ni wakati wa wapenda mpira kusimama na kueleza wazi bila ya woga kuwa kitendo alichokifanya Serge Wawa, beki mkongwe wa Simba kwenda kumkanyaga kwa kumsigina mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi si cha kiungwana na kinapaswa kutolewa adhabu ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hiyo.


Kuna mengi ya kusema kuhusiana na Nchimbi nje ya kuwa mchezaji wa Yanga tu, kitu ambacho kinawazuia wengi kuzungumza kwa kuwa Wawa ni mchezaji wa Simba.


Tukubali Nchimbi ni kijana wa Kitanzania, alikuwa timu kadhaa kabla ya kwenda Azam FC, baadaye Polisi Tanzania na sasa Yanga, huenda siku moja itakuwa Simba.


Pamoja na hivyo kumbukeni Nchimbi ni Mtanzania, kijana wa Kitanzania anayeitumikia Tanzania na kama nilivyosema siku moja huenda akaichezea Simba au kuiwakilisha Tanzania katika ligi mbalimbali za kwingine barani Afrika au hata Ulaya.


Nidhamu ni lazima lakini hata kama ni kazi suala la utu lazima lipewe kipaumbele kwa kutengeneza kizazi cha wachezaji wanaoweza kufikiria kuhusiana na wenzao.


Kwamba, mchezaji aanze kuangalia kama atamuumiza mwenzake atakuwa anatengeneza hasara kubwa katika maisha yake kwa kuwa hayo ndio tegemeo la maisha yake kama ambavyo anavyotegemea yeye.


Mchezaji anayetambua thamani ya kazi ya mwenzake, yake ikatambuliwa hali kadhalika. Maana yake kunakuwa na heshima ya kucheza mchezo wa ushindani unaoepusha watu kuharibiana maisha kwa makusudi.


Katika mchezo wa soka au michezo mingine kuna bahati mbaya, mnaweza kugongana na kuumizana. Kuna mmoja anaweza kumuumiza mwingine na iko wazi, kwamba inaweza kutokea bila ya kukusudia.


Wote tumeona, kwa Wawa hiyo ni tofauti na alikusudia kumuumiza Nchimbi. Unajua, hakuna kipimo cha kuumiza. Amemkanyaga akitumia kiatu chenye njumu, hawezi kuwa na kipimo aumie na asicheze mechi moja tu, badala yake anaweza kumuumiza vibaya na kumsababishia asicheze mechi nyingi au kumuanzishia tatizo litakalokuwa la kudumu ambalo litamsumbua.


Baada ya tukio hilo, mapema nilidhani Wawa angeandika jambo fulani kuonyesha anajutia hicho kitendo cha kipuuzi alichokuwa amefanya, haikuwa hivyo hadi naandika makala haya.


Huenda amedharau, anajua hakuna wa kumfanya lolote. Lakini bado nilifikiri Klabu ya Simba nayo ingekuwa na nafasi ya kuzungumza jambo kuonyesha ina msisitizo wa suala la nidhamu ili kuepuka kuwa na wachezaji wenye tabia za hovyo zinazoweza kuwa tatizo kwa timu pia.


Mazoea hujenga tabia, wachezaji wanaowaumiza wenzao kwa makusudi kuna siku wanaweza kuwaumiza pia hata wenzao kwa maana ya wanaocheza nao timu moja.


Vyombo husika vichukue hatua, Wawa anapaswa kuwa mfano kwa wengine ambao wana tabia hizo ambazo huenda zimejificha. Lakini wakati huu, watakuwa katika kipindi kigumu kwa kuwa teknolojia imepiga hatua ndio maana leo hii kwa mara nyingine baada ya wengine kuumbuka, tunaona Wawa naye akiumbuka.



Bodi ya Ligi na TFF, zina jambo la kufanya katika hili suala. Zisiwe na hofu ya kishabiki, zichukue hatua na ikiwezekana kutoa funzo kwa wengine wajue, hakuna utani katika mambo ya kipuuzi kama hayo.

17 COMMENTS:

  1. Ally Saleh unafiki ni ugonjwa mbaya sana. Lamine Moro alifanya ni dhidi ya Mbeya City. Uliandika ,ulikemea???Au inapotokea tukio dhidi ya timu unayoipenda unakuwa kipofu?Ukitaka kuwa hakimu mzuri basi mizani ya haki ipime kokote sio unapopenda wewe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lamine Moro alifanya nini? nyie hamna akili kabisa kwa hio una support kitendo alichofanyiwa Nchimbi,

      Delete
  2. Ulishupalia penalti ya Simba sasa umekuja kivingine ilimradi tu uendelezeje malumbano ya mechi iliyopita.Si wachezaji wala benchi la ufundi walioongelea hili kwa maana ya kwamba kwao liliisha pale pale uwanjani.Usipende uchochezi katika mambo yasiyo ya msingi.Huenda una ajenda ya siri kwa faida yako si Yanga wa Simba walioongelea hili.Unapokuwa mwandishi si vizuri kuonesha unaegemea upande gani jitahidi kubalance japokuwa ulikumbushia suala la nyuma lililopita na kuvunda

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tatizo la machoko ndio hilo kila mkiambiwa ukweli mnadhani mnataka kubashiwa,kumbukeni salehe aendekezi ujinga

      Delete
    2. Wewe Anonymous at 4:04 PM inaonesha upo tayari kummpa Saleh mkeo amtafune na kuthibitisha uchoko wako maana comment yako inaendana na tabia zako.

      Delete
  3. kwanza ukiangalia vizur mchimbia alinza kuonyesha ubabe na kashikashi kwa wawa ilikuwa lazima kijana abonyezwe kidogo ili kuwa na adabu hzo pia ni mbinu za mechi kubwa kama uliona fainal ya madrid na liver ramos alimbonyeza salah wakapoteana ni mbinu ya mchezo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio maana mie siku zote nasema washabiki wa simba sijui huwa wanaacha akili zao wapi inapofikia hatua ya kukemea mabaya yanayofanywa na wachezaji wao,mie wala nisingeshangaa kama miraji athumani angefanya hivyo..lakini kwa jitu zima kama WAWA Zee lenye midevu kama zote,anafanya ujinga kama ule sio kitendo cha kuvumilia kabisa,,,mtieni kifungo cha maana..

      Delete
  4. Kwa hili Wawa lazima afungiwe na apigwe faini
    Ili kukomesha vitendo vya kihuni

    ReplyDelete
  5. TOKA LINI MBINU YA MCHEZO IKAWA NI KUMUUMIZA MCHEZAJI NI WAPI COACH ANACOACH WACHEZAJI
    KUCHEZA RAFU !!! WAPENZI WA SIMBA HAMPENDI KUAMBIWA UKWELI NA HATA MKIFUNGWA HUWA HAMKUBALI KUA MMEFUNGWA !!!

    ReplyDelete
  6. Ya goswe mwachie gose,tatizo mnaingilia mamlaka au sijui mnajiona mnajua sana,ndo maana waandishi wakibongo siwapendiiiii kama mapolishi

    ReplyDelete
  7. Yondani alifanyiwa nini alipomtemea mate kwasi mate acheni mambo ya kishabiki l!

    ReplyDelete
  8. Umesaha Ramos alivyomfanya M.Sarah? Mbona tuliambia ilikua mbinu nakweli baada yakufanya hivyo Real Madrid walichukua ndoo kwahiyimbinu kwenye mchezo zipo

    ReplyDelete
  9. acha unafiki Saleh bahati nzuri leo umekumbuka kuandika jina lako..blog hii watu huchapisha habari bila kujitambulishwa....mara ngapi Yondani anafanya matukio kama hayo mechi baada ya mechi na huandiki.Mbona Ajib alivyofanyiwa hayo na beki Kagera Sugar hukuandika.Hukuandika pia Yondani alipotemea mate Kwasi..
    Nadhani ungeanza kwanza kwa kuandika Yondani alipaswa kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumzuia Kagere..Kinachoendelea kwenye hii blog ni kutafuta namna ya kuendelea kusheherekea sare...Move on the match was one week ago!

    ReplyDelete
  10. Nakumbuka simba mlixema snaa kwasi alivo temewa mate leo yamewakuta mwaongea ujinga mshabiki wa simba kidgo xna mnajierewa

    ReplyDelete
  11. wewe ndio mjinga hujui hata kinachoongelewa.simba waliongea mchezaji wao kutemewa mate!mpira wa miguu unachezwa kwa miguu...hivyo kukanyagwa kwa mguu inatokea..Mate ya mdomoni tangu lini kwenye mpira wa miguu..suala ni kwamba Saleh huwa kimya pale Yondani anapoendeleza mchezo usio wa kistaarabu tena na tena

    ReplyDelete
  12. Nadhani Saleh ameacha fani yako umesukumwa na mahaba.Ule unaitwa mpira wa miguu wewe ulitegemea sehemu gani yamwili wa Wawa ungemkanyaga Nchimbi wako? Usisahau pia makosa yote uwanjani ya kimpira huamuliwa na Refa au hukaridhika na maamuzi kama ulivyoshindwa kukubali maamuzi ya penalti ya Kagere na kukutea kuwa yondani hakustahili kadi kwa kumdhika
    Kagere? Huwezi kulingamisha kosa la kumkanyaga MTU kwamguu kwemye Moira wa miguu na MTU kuamua kujaza mate mdomoni na kumtemea mwingine kama nyoka kifutu. Bro Saleh wewe mwndishi usiandike vitu kama hujapita chuo cha uandishi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukisoma baadhi ya comments hapa utagundua Aden Rage alikuwa sahihi kuwaita Mbumbumbu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic