January 23, 2016

KIIZA NA NDEMLA WAKISHANGILIA MOJA YA MABAO YA SIMBA....

Hamisi Kiiza amerejea katika ubora wake wa “kucheka na nyavu” baada ya leo kutupia bao mbili wakati Simba “ikiitia njaa” Burkina Faso ya Morogoro katika Kombe la FA linalodhaminiwa na Azam Sports.

Katika mechi hiyo hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kuanza vizuri michuano hiyo ambayo bingwa wake atashiriki Kombe la Shirikisho.

Kiiza alianza kuifungia Simba bao kabla ya Said Ndemla lkufunga la ili halafu raia huyo wa Uganda, akamaliza kazi kwa kufunga la tatu.

Ushindi huo unakuwa ni wa tatu kwa Mganda, Jackson Mayanja ambaye ameingoza Simba katika mechi tatu, zote akimaliza bila ya kufungwa.


Mayanja alianza kuingoza Simba katika mechi ngumu dhidi ya Mtibwa Sugar walipomaliza kwa ushindi wa bao 1-0, Kiiza akiwa amefanya kazi ya “kucheka na nyavu”. Mechi ya pili, Simba ikaituliza JKT Ruvu kwa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic