January 30, 2016




KADI Dk 90+9 Yondani naye analambwa kadi nyekundu na kwenda moja kwa moja vyumbani 
KADI Dk 90+9, daktari wa Coastal aliyeingia kumtibu kipa, analambwa kadi nyekundu
DK 90+5 Mwamuzi anatoa kadi nyekundu halafu anairudisha 
DK 90+4 Yanga wanapata kona, shambulizi kali, Ngoma anapiga kichwa, lakini walinzi wa Coastal wako ngangari kwelikweli

DAKIKA 7 ZA NYONGEZA

Dk 88, Paul Nonga anapiga shuti kali na mpira unagonga mwamba, Coastal wako vizuri wanaondosha mpira
Dk 86, Yanga wanapata kona, Msuva anaichonga, shambulizi ni kali lakini hakuna kitu
DK 81 hadi 83, Coastal wanaendelea kuonekana wako vizuri kwa kucheza kwa juhudi ya juu kabisa
Dk 79, pasi nzuri ya Joshua, Nonga anaiwahi lakini mpira unawahiwa vizuri na kipa
SUB Dk 74, Yanga wanamuingiza Paul Nonga ili kuongeza nguvu
Dk 69, Tambwe na Ngoma wanapoteza mpira, wanashindwa kufunga wakiwa peke yao baada ya krosi nzuri ya Juma Abdul

GOOOOOOOOO Dk 62, Juma Mahadhi, kijana aliyekuzwa na Jackson Mayanja anafunga bao safi kwa shuti kali, Coastal 2, Yanga hawajapata kitu

Dk 54 hadi 59, bado inaonekana mpira umepoteza ladha, nguvu zaidi inatumika zaidi na Coastal kidogo wanakuwa na kasi katika ukabaji

Dk 50 hadi 53, mpira unaonekana kupoteza malengo hasa kiuchezaji na zaidi unachezwa juu au kubutua
Dk 46 hadi 49, Yanga wanaanza kwa kasi wakionyesha wamepania kusawasisha. Lakini Coastal wanaonekana hawana hofu

MAPUMZIKO
Dk 45, Coastal wanacheza taratibu wakionyesha kupania kuumiliki mpira taratibu huku Yanga wakionyesha kuwa na prsha kubwa

KADI Dk 44, Chidiebere analambwa kadi ya njano kwa kutembeza ubabe kila mara
Dk 37, Msuva anapiga krosi ya juu ambayo inakosa mwenyewe na kuwa goal kick

Dk 34, Coastal Union wanaonekana kurudi nyuma ili kuongeza ulinzi wa bao lao hilo moja wanalotaka kumaliza nalo dakika zote 45
Dk 32, Yanga wanapata kona inachongwa na Msuva, mpira unamfikia Ngoma anapiga shuti kali, mwamuzi anasema ni offside

KADI Dk 30, Twite analambwa kadi ya njano kwa kufanya ubabe
GOOOOOO Dk 27, Miraji Adamu anaifungia Coastal Union bao kwa mkwaju wa adhabu baada ya Yondani kuunawa mpira. Alipiga faulo, mpira ukamshinda Dida ambaye anafungwa bao baada ya mechi saba kucheza bila ya kufungwa

Dk 23, Juma Mahadhi anapiga shuti kali kabisa lakini linatoka nje kidogo. Ilikuwa ni baada ya shambulizi kali zaidi la Coastal 

Dk 18, Ngoma anaruka na kupiga kichwa hatari kabisa, lakini kipa anafanya kazi nzuri kabisa na kuokoa

Dk 17 KADI Sabo Yusuf wa Coastal analambwa kadi ya njano kwa kumwangusha Kamusoko
Dk 12 hadi 13 zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na mashuti ya mbali huku hakuna anayelenga lango

Dk 11, Twite anatolewa kwenda kutibiwa nje baada ya kukanyagwa kwa makusudi na Shiboli
Dk 8, shambulizi la kwanza la Coastal Union, Miraj Adam anapiga mkwaju mzuri wa adhabu, lakini anapaisha

Dk 7, pasi nzuri kabisa ya kamusoko, Tambwe anachelewa na Coastal na kuokoa.
Dk 4, Miraj Adam anaruka na kuokoa mpira wa krosi ya Msuva, inakuwa kona, inapigwa na Msuva, lakini haina madhara

Dk 2, Yanga wanapata kona, inachongwa na Simon Msuva, lakini Bakari, kipa kinda wa Coastal, anaruka na kudaka vizuri kabisa
Dk 1, mechi inaanza taratibu sana huku kila timu ikionekana kuwa makini



KIKOSI KAMILI...

1. Deogratias Munishi-30
2. Juma Abdul-12
3.Oscar Joshua-3
4. Kelvin Yondani-5
5. Vicent Bossou-9
6. Mbuyu Twitwe-6
7. Simon Msuva-27
8.Thabani Kamusoko-13
9. Amissi Tambwe-17
10. Donald Ngoma-11
11. Deus Kaseke-4

BENCHINI:
Gk Ally Mustafa-1
2. Pato Ngonyani-15
3. Said Juma-22
4. Matheo Antony-10
5. Paul Nonga-26
6. Salum Telela-2
7. Issofou Boubacar-14

KOCHA MKUU Hans van der Pluijm

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic