Sasa ni misimu sita ya rekodi ya ufungaji mabao ambayo inawajumlisha magwiji Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Wikiendi hii, mmoja kati yao atawania kuwa wa kwanza kufunga boa la 1000.
Messi atakuwa uwanjani katika mechi ngumi dhidi ya Atletico Madrid, wakati Madrid watapambana na Espanyol.
Bao hilo la 1000 litatokana na wao wawili kujumlisha mabao yao tote waliyofunga ambayo idadi take ni 999 baada ya kwa wote jumla kuwa wamecheza mechi ,384.
Messi amefunga mabao 481 katika jumla ya mechi 611, kati ya hizo 432 akiichezea Barcelona na 49 akiitumikia timu ya taifa ya Argentina ambayo yeye ni nahodha kwa sasa.
Ronaldo amepachika mabao 518, alianza kufunga mabao 5 akiwa Sporting Lisbon iliyomlea kisoka kabla ya kujiunga na Man United aliyoifungia mabao 118, akaongeza mengine 340 akiichezea Real Madrid mechi 327. Pia ana mabao mengine 55, aliyoifungia timu yake ya taifa ya Ureno ambayo pia ni nahodha.








0 COMMENTS:
Post a Comment